MAMBO 8 YAKUTOCHUKULIA POA,, KUKWEPA UMASIKINI,,,''wengi wamepotea''
UMEZALIWA KUSHINDA!
Na Prof.Schleiden & Monica Mathias
Kwenye Malengo ya kifedha watu wengi hutamani kuwa matajiri kwa kiasi kwamba kuwa na pesa za kutosha ili kupata kitu chochote wanachohitaji kwa wakati wowote, yahani mtu kupata chakula anachotaka, nguo anazotaka, kusafiri popote anapotaka,kuwa na nyumba yakifahari, kununua gari la aina yoyote anayotaka bila kuwa na shaka na wasi wasi yoyote, wengine matamanio yao yanaenda mbali mpaka kutamani kununua ndege binafsi,kumiliki makampuni makubwa, na mengine kabambe . Ila walio wengi huishia kwenye matamanio tu bila kufikia ndoto zao.
''masikini [kiuchumi] ni mtu ambaye ana upungufu katika mahitaji yake ya msingi ili kuendelea kuishi, hivyo ni mtu anahitaji nguvu ya ziada kutoka nje ya uwezo wake binafsi''
hatuwezi kumwongelea masikini kama hakuna tajiri hivyo basi .......
''Tajiri[kiuchumi] ni mtu ambaye anaweza kupata kitu chochote anachotaka/hitaji kwa wakati kamili kwa kutumia uwezo wake binafsi bila utegemezi wowote.
kutokana na kauli hapo juu kama unaona wewe kula na kuvaa kwako unategemea kutoka nje na kufamfanyia kazi fulani ili akupatie fedha ukanunue unachotaka jua wewe bado si tajiri [kiuchumi] inamaana bado uko tegemezi kiuchumi.
- Takwimu zinaonyesha Duniani kuna watu zaidi ya Billion 7.7 na 5% ndio matajiri tu ambao wanaweza kufanya chochote wanachotaka na utajiri wao uweza kurithiwa, na 15% ni watu wenye uchumi wa kati na wanaweza kupata mahitaji yao yote ya muhimu kwa wakati, na 80% ya watu wote Duniani ni watu maskini ambao kula, kuvaa na kupata chochote wanachohitaji lazima watoke nje na kufanya kazi ama kazi binafsi au kazi za mshahara.
kutokana na hayo SWI GLOBAL COMPANY kupitia GLOBAL FAMILY MEDIA wamekuletea tabia 10 ambazo watu huweza kuziona za kawaida lakini ndizo huchelewesha mafanikio yao na kuleta umasikini.
1.KUTUMIA FEDHA KABLA YA KUZIPATA
Hapa tunamaanisha tabia za kukopa fedha, watu wengi wenye tabia za kujikopesha wamejikuta badae wanaelemewa na madeni jambo ambalo limekuwa kikwazo mtu kupiga hatua mblele kwa ajili ya maendeleo.
Wale wenye tabia za kukopa fedha wakiwa na matarajio ya kupata fedha mbeleni ili wafanye malipo wapo kwenye hali ya hatari kujikuta wanaanguka katika balaa la umaskini. Mara zote fanya kazi kwanza alafu pata hela na fanya matumizi yako, tafuta mkopo ili mradi tu kama ni jambo la umuhimu sana vinginevyo ogopa fedha za mkopo. Kopa ukiwa na uhakika wa malipo kwa wakati.
2. KUFANYA MANUNUZI YASIYO KWENYE MPANGILIO
Kuna watu walikuwa matajiri lakini sasa ni masikini sababu kuu ikiwa ni kuwa walikuwa na tabia za kununua vitu bila mpangilio. Ukiona wewe unanunua vitu bila bajeti, unanunua kitu ili mradi umeona unakihitaji jua umasikini unakuita, ukupata hela zipangilie kwenye mambo ya muhimu asa ukichukua mkopo hepuka starehe fanya vitu vyenye kuzalisha kwa namna hiyo utakuwa umeanza kukimbia umaskini.
3. KUTOWEKA AKIBA/UWEKEZAJI
Waenga wanasema Akiba haiozi, baadhi ya watu maskini leo, ni watu ambao walishindwa kuwa na tabia ya akiba. Akiba sio lazima iwe fedha/vitu vingi, ukijijengea utaratibu wa akiba utaweza kuibuka na utajiri baada ya mda na utaweza kuzitatua shinda mbali mbali zitakazo kukabili.
- Plato alisema ''Utajiri wako hautatokana na mshahara unaoingiza ila kiasi unacho weka akiba kutokana na mapato yako'' Hata ukiwa na mshahara mkubwa kiasi gani kama usipo fanya uwekezaji na kuweka akiba wewe kuwa tajiri utakuwa muujiza mkubwa, tengeneza utaratibu wa kuweka akiba katika uwekezaji kutokana na mapato yako ...... kimbia umasikini.
4. TABIA ZA KULAUMU
Achana na lawama zisizo na faida uepuke umasikini, baadhi ya watu masikini walikuwa hivyo kwa sababu ya kulalamika lalamika wakati wenzao wapo kazini, amini usiamini mtu akijijengea tabia za kulaumu hawezi kamwe kukwepa umasikini,
Tatizo likitokea masikini huwa wahanga ambapo matajiri ulitafakari na kuona namna gani walitumie tatizo kama fursa ya kuingiza kipato hivyo hatuna budi kusema tajiri ataendelea kuwa tajiri na masikini ataendelea kuwa masikini asipo acha lawama za kudumu
5. KUWA NA MARAFIKI WASIO NA MALENGO MAKUBWA
Kuna watu hawanaga mda wa kuwaza maendeleo wenyewe kila mara ni usengenyaji na umbea hawana jipya, wengine ni porojo tu zisizo na faida na hao ndio masikini, epuka umasikini kwa kuwa makini na marafiki ulio nao kama unaona hawakusaidii kuelekea katika malengo yako , una kila sababu kuvunja urafiki huo ili kuepuka umasikini.
- Epuka kutumia mda wako mwingi ukiwa na marafiki ambao hawana malengo makubwa kama ya kwako, ukijikaribisha kwa watu wenye mawazo hasi yahani wenye fikra tofauti na wewe, unapoelekea ni kuwa masikini, ukiwa na marafiki wenye fikra fupi watakufanya ukate tamaa, msomi mmoja Dr. Francisco Red aliwahi kusema "Niambie rafiki yako nikwambie tabia zako'' kumbe unapo tengeneza marafiki hakikisha mnaendana kitabia,kifikra, kimalengo, na hata kiuchumi, kimtazamo vinginevyo mtakuwa watu wa kulalamikiana badala ya kufanya kazi.
6. KUTUMIA MDA MWINGI KWENYE MITANDAO
Chunguza vizuri watu wasio na hela ndo wanashinda kwenye movi, facebook, intagram na you tube nk. hao wanaelekea kwenye umasikini ulio mzito, haiwezekani tajiri kuamka asubuhi anaanza kuangalia movi lakini kwa masikini ni jambo la kawaida sana,
Tukimbie umasikini kwa kuwa na matumizi mazuri ya mitandao, achana mitandao kama haikuikusaidii kuongeza kipato au maendeleo binafsi, kuna watu wanalazimika kukopa fedha kwa ajiri ya kununua movie za vichekesho,,,sasa hapo jiulize vichekesho hivyo vinakusaidia vipi kulipa hilo deni.
Hapo hapo tatizo lingine ni kulala lala, watu wasio na hela wanaongoza kupenda usingizi, kama unataka kukwepa umasikini jua saa ngapi ulale, saa ngapi uamke, sio kulala unapojihisi kulala,,,saynsi inatwambia
- kwa teknolojia ya sasa inabidi kama unabiashara tafuta mbinu ujue ni kwa namna gani utaifanyia mtandaoni ili kuongeza kipato, tunakoelekea karibia shughuli zote zitafanyika mtandaoni,,,sasa wale wenye mawazo ya kibiashara alafu wanatumia mitandao kwa ajili ya vichekesho hiyo ni njia ya kukaribisha umasikini baada ya kupoteza wateja.
7. KUNUNUA CHAKULA
Uzembe ni moja ya vyanzo vikuu vya umasikini, kuna watu ni wazembe wa kupika mtu analazimika kununua chakula cha 20,000/= hotelini wakati alikuwa na uwezo wa kutumia 5,000/= na kujitengenezea chakula bora kabisa akala na kubakiza 15,000/= kama akiba. tabia hii inawakumba hasa wapangaji, lakini ijulikane wazi mtu anaye endekeza tabia hii kukwepa umasikini itakuwa vigumu sana.
Jitahidi uwezavyo kununua chakula kwa wakati ikikulazimu mfano upo safarini, unawahi kipindi au mtihani au ofsini au kazini, nk.. achana na tabia za kununua nunua vyakula kama uchumi wako haujatengamaa, hii tabia waachie matajiri waliokwisha tengeneza miradi ya uwekezaji.
pia kuna kesi ya kununua nunua nguo, viatu, kusuka, na unakuta watu wanaotegemea pocket money [fedha ya matumizi] za wazazi au mkopo wa serikali ndio wanasema tunaenda na fashion [mtindo] huku ni kupotezana kifikra,,,,dada kama unadhani kubadilisha msuko kila wiki, viatu kila siku, nguo kila siku ndipo utapata mchumba mwema kwa hali hiyo unajidanganya ila unachofanya ni kuongeza namba ya wanaokutamani kuliko wanao kupenda, mchumba mwema utampata kutokana na tabia zako za kila siku na staili [falsafa] yako ya maisha [tusikwazane]
bajeti matumizi ya fedha fanya uwekezaji,,,mitindo waachie matajiri,,,maisha ya kuigiza uleta umasikini, lengo letu ni kupambana na umasikini,tunalazimika kujali mafanikio yako hakuna lisilowezekana.
8. KUTOSALI/SWALI
Hii ndiyo pointi kuu kuliko zote imekaa mwisho ili ikumbukwe zaidi, watu wengi masikini wanashindwa kumtanguliza Mungu katika mambo yao ila wakipata matatizo ndo wanakimbilia makanisani na misikitini tutafuta miujiza. Hili ni tatizo kubwa, Usingoje kupata shida ndo umwombe Mungu fanya hivyo iwe kawaida yako kumtanguliza Mungu. ijue ratiba ya kwenda mbele za Mungu kadri ya dini yako na jitahidi kuitimiza hakika utabadilisha maisha yako.
Usipo anza na Mungu kwenye Mradi wako, tegemea kuna jambo siku latakuja enda mrama....
Kumtanguliza Mungu ni pamoja na kujipenda yahani kujali afya yako,,,fanya vipimo kila mara usingoje kuumwa na ishi vema kadri ya mafundisho ya dini yako kwa kufanya hivyo Mungu atakubariki nawe utajaa baraka za Mungu na utafanikiwa sana kwenye shughuli zako zote
'TUNACHUKUA FURSA HII KWA KUJUMUIKA NA GLOBAL FAMILY KAMA MWANAFAMILIA......KUNA MAKALA NZURI SANA TUMEZIANDAA KWA AJILI YAKO ENDELEO YAKO,
NI SISI TUNAOJALI MAFANIKIO YAKO @global_family2020
Tunaendelea na kuandikisha watu wenye vipaji (TALENTS) mbali mbali kupitia online system, lengo letu ni kuwa support iwezekanavyo ili waweze kufikia ndoto zao,, ni sisi tunaofatilia maendeleo yako mwisho wa usajili utakamilika itakapofika namba ya watu wanaohitajika. USIKOSE FURSA HII HAITATOKEA
TENAπ€π€π€ ...... π CLICK HEREto attend online for your self .Unaweza ku-comment!, kuuliza Swali lolote na ku-share.
Ni sisi tunaojali mafanikio yako!
Asante sana Monica na Prof... Nimejifunza mengi naendelea kufuatilia
ReplyDeleteNi kweli kabisa....
ReplyDeleteAsante Global Family
Namejifunza vitu
Amina sana Global Family Foundation naendelea kufuatilia πππππ
ReplyDelete