MBINU KUU 4 ZA KUWA MBUNIFU KITAALAMU ZAIDI
DIRA YA MAFANIKIO
Na Prof.Schleiden & Monica Mathias
Katika maisha yote, mtu yeyote ili kufanikiwa ni lazima kuwa na ubunifu kwa kiwango cha juu, kutokana na ubunifu tunaweza kuongeza wateja katika biashara, tunaweza kugundua mashine mpya na kuongeza uzalishaji, tunaweza kutumia nguvu kidogo katika kufanya kazi kubwa, tunaweza kufaulu katika mitihani, unaweza kupata mchumba afaaye, n.k....
Mataifa makubwa kiuchumi Duniani ndiyo mataifa yanayoongoza katika idadi ya wabunifu,Rais mstaaf Barack Obama ananukuliwa '''In order to conquer the world we must first encourage creativity among the USA citizens''---2013 [Ili tuweze kutawala kidunia ni lazima kwanza tuchochee ubunifu zaidi kwa wananchi wa Marekani]
Ni imani yetu tukiongeza ushawishi katika kuchochea ubunifu katika waafrica hasa watanzania ndio itakuwa moja ya sababu kubwa ya kimaendeleo na kufutilia mbali utegemezi tulio nao, mfano; Tanzania ni moja kati ya mataifa 20 Duniani kwa kuwa na Utajiri mkubwa wa rasilimali, cha ajabu Tanzania ni moja ya Mataifa 20 Yanayoongoza kuwa na madeni makubwa na kuwa na Raia masikini. Imani yetu ni kwamba tukiweza kuchochea ubunifu, tutaweza kuifanya nchi yetu kuwa Taifa kubwa lenye nguvu na linalogawa misaada na mikopo kwa mataifa mengine Duniani.
Ili kuwezesha jambo hilo GLOBAL FAMILY FOUNDATION imekuletea mbinu kuu 4 za kutumia ili kuwa Mtaalamu wa ubunifu katika sekta yoyote na hivyo kuifanya kazi yako ikulipe zaidi na zaidi.
✈MBINU KUU 4 ZA UBUNIFU
1. Chagua Kitu Unachokipenda
Mda wetu wa kuishi Duniani ni kidogo sana, hivyo hatuwezi kuwa wataalamu katika kila kitu, hivyo hatuna budi kufahamu nini tunaweza kufanya? na tunaweza kufaidika vipi?,,,,Ili tuwe washindi ni lazima tuchague jambo moja/mawili/matatu ambayo tuna uhakika na kuyafanya kwa uwezo wote na kuja na mafaniko tuliyo yatarajia.
Watu wengi wanapata taabu sana kwa sababu ya tamaa, hivyo ili kuwa mtaalamu katika ubunifu ishinde tamaa mfano, kama ni mziki fanya mziki, kama ni uchoraji fanya uchoraji, kama ni kuigiza fanya hivyo, kama ni sayansi fanya sayansi, kama ni mpira cheza mpira,
wahenga wanasema ''Mtaka yote kwa pupa hukosa yoteeeπ€π,,,,'''Swala wawili walimshinda fisi'' tujiepushe na tamaa ya kufanya vitu vingi bila uwezo, tunaweza kufanya mambo machache yenye faida zaidi na kuyafanya vizuri tuwe na tabia ya simba yaani kamwe tusiachene na jambo lenye faida kubwa kabla hatujalikamilisha.
wahenga wanasema ''Mtaka yote kwa pupa hukosa yoteeeπ€π,,,,'''Swala wawili walimshinda fisi'' tujiepushe na tamaa ya kufanya vitu vingi bila uwezo, tunaweza kufanya mambo machache yenye faida zaidi na kuyafanya vizuri tuwe na tabia ya simba yaani kamwe tusiachene na jambo lenye faida kubwa kabla hatujalikamilisha.
usitegemee leo upo huku, kesho kule, kesho kutwa huko,,kwa hali hii huwezi kabisa kunufaika na ubunifu wako yahani shughuli zako zitakuwa nusu nusu. Siku zote ukitaka kuwa Mbunifu makini na uliyebobea [professional] ogopa tamaa!! fanya jambo kwa wakati na hakikisha unatafiti kujua katika kila jambo unapata faida kiasi gani??? [''don't be busy for nothing'']
2. Wekeza katika Kuwaza na Kutenda
Watu wengi wana mawazo mazuri mno yenye kujenga na kuleta maendeleo, lakini changamoto inakuja kwenye kuyafanyia kazi mawazo yao ili yalete faida kama inavotegemewa wanakwama kwa kukosa kuweka misingi imara, kitendo hiki kina wakwamisha ndugu zetu wengi ili kuwa mbunifu mzuri ni lazima kufikiria sana John Abraham alisema ''Kuwa na fikra mithili ya dunia lakini matendo kama kijiji...''[Think Globally, act Locally].
Ili kuwa mbunifu lazima uwe ni mtu anayefikiria sana, tukifikiria sana mara kwa mara hatupotezi chochote ila ndipo tutafaidikaa zaidi. Mwanafalsafa Albert Einstein aliwahi kusema ''Nikipewa dakika moja kutoa suluisho kwa tatizo lililotokea nitatumia sekunde 55 nikifikiria na nitatumia sekunde 5 kutoa suluisho''' [In case I'm given 1 minute to solve a problem I will use 55 Seconds thinking then I will use 5 seconds providing a solution]
Tumia muda mwingi kufikiria katika ukimya wa ndani,,Mwandishi mahiri wa vitabu Edius Katamugora aliwahi kusema ''Ukipata wazo la faida kaa kimya litafakari, usikurupuke katika ukimya utoka makubwa'' [Once you get a best Idea be silent make a deep thinking on it, don't rush, from silence the great matters rise]
Pia Prof. Honest Ngowi aliwahi kusema ''Watu wenye busara huongea jambo pale tu wanapopaswa ila wajinga uongea kila wakipata nafasi ya kuongea'' [Wise people speak only when are to speak but fools speak whenever get an opportunity to speak]
Mpendwa mwanafamilia lengo letu ni kukuwezesha uwe mtaalamu katika ubunifu, ili kuwezesha jambo hilo, ogopa kuishi kwenye matamanio bila kushughulika mfano: usitamani tu kumiliki gari ila fahamu ufanye nini umiliki gari, usitamani tu kumpata mpenzi mwema ila fahamu pia nini ufanye ili kumpata mpenzi mwema, usitamani tu kupata GPA ya 5.0 ila pia fahamu GPA hiyo unapataje na utafaidika vipi?
usiogope,,, kila kitu kinawezekana, la msingi ni kila siku kujiwekea walau dakika 10 za kujitafakari na kuona unaendeleaje katika kuishi ndoto yako??? siku ina dakika 1440 usiwe mchoyo kwa kujinyima walau dakika 10 za kujitafakari kila siku, Nelson Mandela alisema mtu huanza kuwa masikini anapoanza kuifanyia nafsi yake uchoyo binafsi'' baada ya tafakari [kuwaza] mipango utakayoipata iweke katika matendo, trust me! [niamini] utashangaa unaweza jambo aambalo hukutegemea yahani utaishangaza jamii!!
3. Jifunze vitu vipya vinavyoendana na Jambo lako
Hapa ndiko kuzuri zaidi, ukitaka kuwa mbunifu usichoke kujifunza, mtaalamu wa ubunifu ni mtu wa watu,, kama unataka kuwa mbunifu huna budi kujichanganya na watu kamwe usimzarau mtu,ishi vema na kila mtu na tafuta kufaidika na kila mtu hivyo kuwa na utamaduni wa kujifunza jambo linaloendana na ubunifu wako kutoka kwa watu.
Usipokuwa na uelewa vizuri kuhusu jambo lolote hakikisha unamtumia vizuri kila mtu kwa kupata faida, tujitahidi kuepuka kuwa na marafiki wanafiki wasio na mchango katika ubunifu wetu lakini tusikome kujifunza mambo mengi.
Kama unataka kuwa mbunifu wa hali ya juu, tengeneza adhira yako,yaani kuwa na watu ambao kwa mda wowote wanaweza kukusaidia katika kuendeleza ubunifu wako, ni heri kutokuwa na rafiki kabisa kuliko marafiki wa misimu ...Jack Ma Bilionea wa kwanza wa kichina aliwahi kusema '''Kama unaona mita ya kupima thamani ya rafiki zako inasoma hasi, vunja huo urafiki baki na Mungu wako'' [If you see the data meter of friendship is reading a negative value , Knock down friendship and stay with GOD'' huyu bilionea ni moja wa wabunifu wakuu wa Dunia hii na ndio mmiliki na mwanzilishi wa kampuni la ALIBABA,
Kama unataka kuwa mbunifu wa hali ya juu, tengeneza adhira yako,yaani kuwa na watu ambao kwa mda wowote wanaweza kukusaidia katika kuendeleza ubunifu wako, ni heri kutokuwa na rafiki kabisa kuliko marafiki wa misimu ...Jack Ma Bilionea wa kwanza wa kichina aliwahi kusema '''Kama unaona mita ya kupima thamani ya rafiki zako inasoma hasi, vunja huo urafiki baki na Mungu wako'' [If you see the data meter of friendship is reading a negative value , Knock down friendship and stay with GOD'' huyu bilionea ni moja wa wabunifu wakuu wa Dunia hii na ndio mmiliki na mwanzilishi wa kampuni la ALIBABA,
4. Tambua Fursa na Zitumie
Sifa moja kuu ya mbunifu ni kuacha sikio lake na jicho lake wazi kuruhusu fursa mpya ziingie, ili kuwa mtaalamu wa ubunifu tujitahidi kujifunza kugundua fursa zinazotokea na tuzitumie hii itatusaidia kukuza ubunifu na kugundua vitu vipya......likitokea tatizo usiwe wa kwanza kulalamika bali ngalia ni kwa namna gani utatumia ubunifu wako katika kutatua tatizo husika.
''Tatizo likitokea masikini ndio muhanga lakini tajiri uangalia ni kwa namna gani atumie tatizo hilo kujitengenezea faida'' kumbe mtu mbunifu hana budi kuhakikisha kila tatizo litokealo kuliangalia kwa jicho la faida ili kujiingizia kipato,, na kwa namna hiyo kuzidi kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindi na kukuza ubunifu wake lakini pia kukuza kipaji chake,,,
Usiogope kutumia fursa, ipokee fursa itakuongezea ubunifu na utaweza kutengeneza vitu vikubwa zaidi, Mwanasayansi mahiri Kepler aliwahi kusema '''Ubongo wabinadamu unatajiri mkubwa kiasi kwamba akitumia 60% ya ubongo wake anaweza kubadili mwonekano mzima wa Dunia''
Hatuwezi kutenganisha kipaji chako na Ubunifu,,,,namna unavyozidi kuwa mbunifu ndivyo unazidi kukuza kipaji chako na kupata faida kubwa zaidi ,,,,,
πASANTE SANAπ TUNACHUKUA FURSA HII KUKUKARIBISHA KATIKA MAKALA ZINAYOFUATA KUHUSU MAISHA YA WABUNIFU WAKUBWA DUNIANI KAMA JACK MA, JEFF BEZOS, MARK ZUCKERBERG...N.K, NI SISI TUNAOJARI MAFANIKIO YAKO. KARIBU TENA KATIKA GLOBAL FAMILY FOUNDATION
Tunaendelea na kuandikisha watu wenye vipaji mbali mbali kupitia online system, lengo letu ni kuwa support iwezekanavyo ili waweze kufikia ndoto zao,, ni sisi tunaofatilia maendeleo yako mwisho wa usajili utakamilika itakapofika namba ya watu wanaohitajika. USIKOSE FURSA HII HAITATOKEA
TENAπ€π€π€ ...... π CLICK HERE to attend online for your self .
Unaweza ku-comment!, kuuliza Swali lolote na ku-share.
Ni sisi tunaojali mafanikio yako!
TENAπ€π€π€ ...... π CLICK HERE to attend online for your self .
Unaweza ku-comment!, kuuliza Swali lolote na ku-share.
Ni sisi tunaojali mafanikio yako!
Hongereni sana Global family foundation kwa kazi nzuri mnayoendelea kutuletea...
ReplyDeleteHongereni sana kwa kazi mnayofanya Global family foundation..
ReplyDelete.
Thanks very Much Global family foundation, we are looking forward with your vision and missions in East Africa.#together_wecan
ReplyDeleteNashukuru sana Global Family Foundation kwa uzalendo wenu....Tupo pamoja kwa maendeleo...ikiwezekana tunaomba huduma zenu zifike mashuleni na vyuoni, mtawasaidia vijana wengi
ReplyDeleteNimesoma neno kwa neno...nimejifunza Mengi...Tunaomba kampuni lenu litufikishie huduma zaidi..tutachochea maendeleo sana katika Africa
ReplyDeleteProf. Schleiden umetisha sana keep it up, tupo pamoja kwa ajili ya ushindi (Naomba kujua historia za matajiri wakuu wa Tanzania na Dunia...ππππ
ReplyDeleteThanks global family mambo mazuri
ReplyDelete