KIJANA MIAKA 18-35 USIKOSE HII

,MAMBO MUHIMU AMBAYO KIJANA ANATAKIWA KUFANYA 

       Na Prof. Schleiden & Monica Mathias

Katika maisha ya binadamu hakuna kipindi kigumu sana kama kipindi cha miaka 20 mpaka  30 kipindi hiki ndio kipindi chenye utata, hapa kijana anaweza kujenga maisha yake au kuyabomoa na walio wengi wanaanguka hapa, lakini pia wengi huanza kufanikiwa kuanzia hapa wote kutegemeana uwezo wao na maono yao yalivyo.

ikumbukwe katika miaka 20-30 kijana  ndipo anakuwa anamaliza elimu ya sekondari, ndipo ana anakuwa chuo kikuu, ndipo anaingia kwenye mahusiano ya mapenzi, ndipo anahitimu chuo kikuu, ndipo anaangaika kutafuta ajira, ndipo ana kuwa na mchumba pia ndio kipindi wengine huanza maisha ya kujitegemea kuacha familia za wazazi, wengine hufunga ndoa hapa, pia hiki ni kipindi kijana anaanza kutegemewa na familia ya wazazi wake na jamii. Kwakweli kipindi hiki sio cha mchezo ni kipindi cha kutumia akili nyingi na ushauri mwingi wanao kichukulia poa kinawaachaga vinywa wazi maisha yote.
Vijana wa Tanzania
Ndugu Mwanafamilia, Global  Family Foundation imekuletea Mambo muhimu ambayo kama kijana unalazimika uyafanye kwa ajili ya faida yako binafsi ama kwa ajili ya faida ya jamii na taifa kiujumla, tunamatumaini utakuwa umeshaanza kuyafanyia kazi ila tunazidi kukuangazia mwanga zaidi ili kurahisisha njia yako ya mafanikio. KARIBU!

Kijana ni mtu mwenye umri kati ya miaka 18-35 kulingana na katiba ya Tanzania. Lakini kidunia kijana anachukuliwa kuanzia umri wa miaka kuanzia 15-28. Hivyo, kuna mambo makuu ambayo mtu anatakiwa kufanya wakati wa ujana wake. Na mambo hayo ni pamoja na;

KARIBU


1. Kupata elimu
Tunapo zungumzia elimu tunamaanisha ujuzi maili ambao utakusaidia kutatua changamoto mbalimbali na kuwezesha shughuli za maendeleo, hivyo kufikia miaka 18 tunaamini unakuwa tayari umepata  elimu ya msingi na ya sekondari na unakuwa unaelekea kwenye elimu ya chuo baada ya hapo kijana ataweza kutumia elimu hiyo aliyoipata katika kuendeleza kipaji au taaluma nyingine ambayo anaweza kufanya. Kila kijana anatakiwa kupata elimu hiyo kwani ni muhimu sana katika  kuendeleza maisha yake kwa dunia sasa.

Ili kijana ufanikiwe katika jambo lolote lazima uwe na ujuzi kamili katika jambo hilo, vinginevyo utateseka sana kufikia ndoto zako, pia epuka kumdharau mtu yeyote, kila mtu anaweza kukufundisha kitu kipya chenye manufaa makubwa kwako na kwa mafanikio ya familia na  jamii  kiujumla, kujifunza hakuna mwisho msomi mmoja aliwahi kusema mtu unapoona umeacha kujifunza ujue hapo umeanza kupunguza kufikiri na kifo kimeanza kukusogelea.

2. Kuwa na mali za kudumu (fixed assets).
Kijana katika umri wake anatakiwa awe na uwezo wa kumiliki vitu vya kudumu kama vile vifaa vya kazi,ardhi au kiwanja, nyumba na kadhalika. Hii inasaidia sana kwa maisha ya baadae ya uzeeni kwani unakuwa umeandaa mazingira yako tayari ambapo itapelekea maisha kuwa mazuri baadae. 
Ni vema kijana kuwa na mali binafsi

Ramani ya nyumba nzuri ya kijana
miaka 18-35

Kijana jifunze kuwa na maono makubwa epuka tabia za utemegemezi yaani jitahidi na wewe kuwa na uwezo wa kusema hiki ni cha kwangu sio tu vitu vyote ulivyo navyo ni vya watu wengine na wewe kuwa na mali zako unazo miliki.



3. Kuwa na mahusiano ya kweli na ndoa
Hapa vijana wengi ndipo tunapotezana sana kwani tunajikuta muda ambao ni sahihi wa kuwa katika mahusiano ambayo ni ya kweli na kudumu tunakuwa katika mahusiano yasiyo ya kweli na kujikuta tunapoteza mda mwingi katika kitu ambacho hakikuwa sahihi kabisa. Katika umri wa kijana ambao ni miaka 18-35 kijana anatakiwa kuwa na sehemu moja ambayo amesimamia katika mahusiano ambayo itapelekea kuwa na ndoa kamilifu na kuanza familia ya kuzeeka nayo.

Kama ilivyo tangulizwa mwanzo hiki ni kipindi cha kuwa makini sana na kutumia akili nyingi na ushauri mkubwa hasa kwa upande wa mahusiano ya kimapenzi inasikitisha vijana wengi wamedanganyika sana katika kipindi hiki katika swala la mahusiano, walio wengi wanawakataa wapenzi wao waliokuwa na dhamila ya kufikia katika ndoa. 

Baadhi ya vijana wanaowapotezea wale wenye mapenzi ya kweli na baadae ndio wanaishi maisha magumu, wengine wanaachwa na wapenzi wao na wanabaki wakiyaona maisha magumu wanakosa la kufanya wanazeekea kwa wazazi wao, baadhi ya vijana wanafika miaka 30 bila kuwa na mwelekeo wa ndoa kwa sababu waliwapotezea wale waliokuwa na mapenzi ya kweli kwao na kuwaona hawafai  kumbe hawakuchukua nafasi kuwachunguza nia na dhamila zao na hata kuona maono na mipango yao ya badae.

Fursa ikipotea, hairudi
Waenga wanatwambia unaweza ukawa na mtu  wa maana sana kwenye maisha yako anayekusaidia kila kitu na kukwambia mambo yake yote na unaweza kuwapata kirahisi lakini lakini ikitokeaa ukampotezea katika mambo anayokwambia ukisha mpotezaa huyu mtu unaweza usimpate tena mtu kama huyo katika maisha yako yote,  hivyo kwenye swala la kuishi na watu kama kijana jiadhali sana na kutopotezea watu, kuwadanganya na kuwajaribu watu ulionao karibu maana unaweza ukafanya kitu cha kawaida lakini rafiki yako hakakiona kuwa kitu kikubwa sana na kikawakwaza.

Pia kama kijana ni muhimu kutambua thamani na lengo la kila mtu uliye naye katika maisha yako, kuna marafiki unao ni kwa ajiri ya kukufundisha vitu,  ila kuna watu ni kwa ajili ya kukujaribu na kukuimarisha ,kuna watu unao ni kwa ajili ya kukufanya ushindwe ,pia kuna watu waonekana kama wanakupenda nakukujari ili maisha yaende mbele katika shughuli mnayofanya lakini pia kuna mtu mmoja tu yupo ili kuwa nawe kwenye ndoa na huyo mtu sio rahisi kumtambua kama hauko makini na humtangulizi Mungu katika fikra na matendo yako. 
Hii sio safi kwa kijana

Unapokuwa kwenye jamii ya watu wengi unaweza kuwa na mtu mkawa kwenye mahusiano ukadhani  anawaza kuwa nawe mpaka kwenye ndoa kumbe yeye hana fikra fikra hiyo kabisa bali ana mtu wake mwingine mbali, hivyo ukidanganywa na anavyokujali na kukupa mda wake utajikuta unampotezea yule aliyekuwa na mapenzi ya kweli, akikuacha ndipo utaanza kufahamu maana ya maisha magumu

kumbe kama kijana huna budi kuhakikisha unafahamu lengo la kila mtu uliye naye  kwenye ukaribu wa maisha yako hasa kwenye mahusiano ukienda hovyo hovyo bila utafiti na uchunguzi wa kina utajikuta unapoteza mpenzi wako halisi kwa sababu ya maamuzi ya ajabu Jifunze kuchukua nafasi na kumdadisi na kumchunguza uliye naye kwenye mahusiano watafiti wa maswala ya kijamii wanasema ni chini ya 30% ya watu wote wanaoingia kwenye mahusiano huweza kufika kwenye ndoa na hivyo na hakika kabisa kusema sio kila mahusiano yanalenga kufika kwenye ndoa na kama kijana ukiona upo kwenye mahusiano na hayalengi kufikia ndoa huna budi kujitafakari na kuchukua hatua kuliko kuja kumpoteza mwenye mapenzi ya kweli [Dont loose gold while counting stones]. Na inasemekana mtu anayekupenda kweli na anaona unampotezea kila mara atajitahidi kukusisitiza katika swala hilo ila ukiwa Mgumu kuelewa anaweza kukuacha ila hawezi kukuacha kabisa wala kukusahau maana alikuwa na upendo wa dhati kwako.

Unaposali kumuomba Mungu mchumba mwema pia tumia akili yako  na fungua milango yako ya fahamu na kuwachunguza watu unaoishi nao ,marafiki, wanaosema wanakupenda wafanyie utafiti na uone dhamili zao kamili na maono yao na malengo yao , historia zao, uwezo wao na namna gani wanakiishi kile wanachokwambia, na kukujali na sababu za kufanya hivo.
Mfanye Mungu kuwa wa
kwanza katika kila kitu

Hiyo haitoshi muombe Mungu kila siku, mchumba mwema hatoki mbinguni ni binadamu kama wewe,,,,,Amini haitakuja kutokea Mungu kuja kwako kwa Mguu na kukwambia mchumba wako ni huyu,,,,,,,Kama kijana ni vema kabisa kumtambua mapema mchumba wako na kuanza kuwa naye karibu na kupangilia mipango ya maisha sio kila siku ni vichekesho na burudani na ukiona mpenzi wako hakushirikishi kikamilifu mipango yake ya  badae na  anakuficha mambo yake, tafakari na chukua hatua.

4. Kuwekeza sehemu yoyote ya maendeleo


Katika umri wa kijana mtu anapaswa kuchangamkia fursa za maendeleo na kuweza kuwekeza huko kwa ajili ya mambo ambayo yanatakiwa kutimizwa kwa huo wakati wa ujana  na hata baadae. 
Kijana jifunze kuwekeza
kuanzia sasa

Kijana yeyote yule hapaswi kupoteza fursa zinazokuwa katika mazingira anayoishi kwani zinakuwa mikononi mwake, kwani tunashuhudia vijana walio wengi waliokubali kufata na kushughulikia fursa zilizowatokea wameweza kupata mabadiliko makubwa katika maisha yao.

Leo hii kuna fursa nyingi lakini baadhi ya vijana wanakuwa wagumu kuzitambua ila wengine wanachagua kazi, hii sio poa kabisa kijana inabidi uwe tayari kufanya kazi yoyote halali inayo kidhi vigezo kiafya na kisheria ili ujipatie kipato binafsi,,kuna baadhi ya vijana wapo  vyuoni lakini hawakomi kuwa na aibu kuomba hela za matumizi kwa wazazi ... tunapofanya hivyo tunajishusha adhi na elimu tuliyo ipata hatuitendei haki. kwakweli  kijana wa chuo kikuu inabidi awe mstari wa mbele kuwasaidia wazazi, na kuwasaidia ndugu zake hio ndio maana ya kuwa mtu mzima.

5.  Kuepuka starehe zisizokuwa za muhimu
Kijana asiye na starehe sana
ndio anayefanikiwa
Kwa huu upande, vijana tulio wengi tunapenda starehe ambazo kiuhalisia hazina manufaa kwa maisha yetu ya baadae. Kwa kawaida binadamu ni lazima tupate furaha na kuweza kuburudika, lakini kuna muda unafika starehe hizo za kuburudika inabidi kupunguza hii inaweza kusaidia kupunguza baadhi ya matumizi ambayo sio ya lazima na kutakuwa na uwezekano wa kuongeza kipato kikubwa kwani matumizi yatapungua kwa asilimia fulani.



7. Fungua akaunti ya pesa
Kwa kawaida katika umri wa ujana lazima kila mtu awe na matumizi ya pesa hivo tunapaswa kuwa na akili ya namna ya kutunza pesa kwa ajili ya matumizi yake. Hivo ni vizuri sana kwa kila kijana kuwa na akaunti ya pesa na hii inasaidia katika kuweka pesa kwa ajili ya akiba ya maisha ya baadae.

Kijana kama baba/mama mtarajiwa jifunze kuwa na akiba ya fedha na jua njia nzuri ya kutunza ili sio kila shida  ya fedha inayotokea lazima uombe kwa mzazi,  kama mtu mzima inabidi uanze kujitengenezea utaratibu wa kumaliza shida ndogo ndogo, vile vile ukiwa na marafiki unaweza kuwatumia kumaliza shida ndogo ndogo kama kusaidiana na hapo ndo umeanza kuishi maisha ya kiutuuzima.

8. Kuwa na marafiki wenye tija
Marafiki wa faida ni faraja kwa kijana
Hapa kinachozungumziwa ni kuwa na marafiki wenye faida kwa maisha yako, kwani inajulikana sio kila rafiki ataweza kuwa na faida kubwa kwako. Hivo kwa katika kipindi cha ujana tunatakiwa kuwa makini na marafiki tulionao inatakiwa wawe ni marafiki wenye kuwa na changamoto za maendeleo, wenye kukukosoa pale utakapo anguka na wenye uwezo wa kukusaidia popote pale na kwa kitu chochote kile.
Vijana wazuri huwa na
marafiki wanaopendana

Kijana ni jambo la msingi na ulazima kuwa na marafiki, lakini pia ni vema kabisa kujua aina za marafiki ulionao na umuhimu wao maana sio kila unamuona kuwa rafiki ni rafiki kweli wengine wanataka ufanikiwe lakini wengine wanakuchunguza ili wakukwamishe kwenye ndoto zako, 

Kijana usisite kuuvunja urafiki wowote usio na tija kwako, kwa ajili ya mafanikio yako.

9. Anza kuishi ndoto na malengo yako
Inajulikana wazi kuwa kila mtu ameumbwa na kitu ambacho anatakiwa kukiishi na kuweza kukifanya katika dunia hii. Hivo katika umri wa kijana ni vyema kila mtu akaweza kuishi na kufanya ndoto yake kwani ndio wakati mzuri wa kufanikisha ndoto na malengo yako.

Hakikisha maneno yako, matendo yako na fikra zako vyote vinaendana na ndoto zako pamoja na malengo yako, katika kipindi hiki anza kutengeneza uhusiano na watu wakubwa pamoja na watu waliofanikiwa tayari, hawa watu  watakusaidia kama kijana kwenye kukupatia ushauri na mambo mbali mbali maishani vile vile utaweza kuwapata ambao watakusaidia kupata kazi kama bado unasoma.

KIJANA ndio nguzo ya familia, jamii na taifa  hivyo unavyo pambana ndivo unaleta maendeleo, kumbuka wewe ni wa pekee kabisa unavochezea ndoto yako unawakwamisha wengine, maana kuna watu wanahitaji kutumia mafanikio yako ili nao kufanikiwa.




πŸ”‚asante, karibu tenaπŸ”‚
MPENDWA GLOBAL FAMILY FOUNDATION INAJALI MAFANIKIO YAKO
TUNAZIDI KUKUSHUKURU KUENDELEA KUWA NASI
⌚#ISHI NDOTO YAKO LEO⏰


Tunaendelea na kuandikisha watu wenye vipaji (TALENTS)mbali mbali kupitia online system,  lengo letu ni kuwa support  iwezekanavyo ili waweze kufikia ndoto zao,, ni sisi tunaofatilia maendeleo yako mwisho wa usajili  utakamilika itakapofika namba ya watu wanaohitajika.  USIKOSE FURSA HII HAITATOKEA
 TENA🎀🎀🎀 ...... πŸ‘‰ CLICK HERE to attend online talent Registration easily .

Unaweza  ku-comment!, kuuliza Swali lolote na ku-share.

Ni sisi tunaojali mafanikio yako!



CONTACTS:
phone call:  +255747787796
WhatsApp: Just clickπŸ‘‰ HERE   To automatically open whatsApp online service
Website: πŸ‘‰Click HERE    To open the Site


Email: πŸ‘‰ Click Here










Comments

  1. Thanks very Much Monica and Professor I salute you! May your project be extended to UDSM Also
    Thanks

    ReplyDelete
  2. Asante sana, nimejifunza mengi. Napenda Sana kazi mnayofanya kwakweli ntakuwa mchoyo was fadhila nisipo kushukuru Mrs. Monica na Profesa scleiden Mungu awabariki mno naendelea kufatilia.

    ReplyDelete
  3. Agnes Johannes ZabronApril 2, 2021 at 9:12 PM

    Brother Octavian,,, I appreciate your Efforts in Creating useful Foundation base for the Youths and The Tanzanians πŸ™πŸ™ God Bless SWI🌍 God Bless Octavian😎 God Bless Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ God Bless the World 🌎

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

HISTORIA YA SAID SALM BAKHRESA

MAMBO YALETAYO FURAHA YA KWELI MAISHANI

MBINU KUU 4 ZA KUWA MBUNIFU KITAALAMU ZAIDI