FUNZO KUU LA KUFANIKIWA ATOA JACK MA

BILIONEA  MBUNIFU ZAIDI WA KICHINA

Na Prof.Schleiden & Monica Mathias
Jack  Ma  hakuwa mtu mwenye akili nyingi sana , alikataliwa alidharaulika, alichekwa sana katika maisha yake ya mwanzoni, lakini leo hii ukiwa unahesabu matajiri  wakubwa Duniani ni kosa la jinai kumsahau Jack Ma  bila shaka wewe kama ni mtumiaji wa internet basi wewe sio mgeni kusikia neno 'ALIBABA' Leo hii ni moja ya makampuni 20 makubwa sana Duniani, mwanzilishi na mmiliki ni Jack Ma Kumbuka China ina zaidi ya Raia Bilion 1.3 yaani 1,300,000,000 na Jack Ma ndo Tajiri namba moja hapo sasa ujue alitumia ubunifu kiasi gani............

Global Family Foundation Imekuletea historia ya Bilionea huyu ili kukuonyesha mtu anayetafuta kufanikiwa maishani namna gani inabidi awe, tukiwa na maana utajiri / mafanikio ya kweli hayaji kwa bahati nasibu, 🔜Karibu sana tuna matumaini utajifunza kitu.


""Kama unataka kufanikiwa huna budi kufatilia historia za watu waliofanikiwa""__Prof. Schleiden


Jack Ma  ni Raia wa china kazaliwa 10/09/1964, alizaliwa kwenye familia ya kawaida kabisa, na alisoma shule za kawaida bahati mbaya hakuwa na akili nyingi, sana kama walivyo matajiri wengine, alishindwa mitihani mara kwa mara na pia alishindwa mitihani ya kujiunga na chuo mara tatu, aliomba kujiunga na Harvad University mara kadhaa alishindwa, maisha yakamuwia magumu akatafuta vibarua katika uchina kote akakosa.

Badae alifanikiwa kusomea shahada ya ualimu mwaka 1988 huko china na baada ya hapo alitafuta kazi akakosa kabisa, aliomba ualimu katika Harvad University akakataliwa, akaomba kazi kwenye makampuni akakosa, akaomba kazi ya upolisi akaambiwa hafai, alienda na wenzake 23 kuomba kazi hotelini wenzake wote wakapata lakini yeye tu akakosa.

Baadae akapata kibarua cha kuwatembeza watalii, siku moja alimtembeza mtalii mmoja akawa ameshindwa kutamka jina lake lake la ubatizo la Ma Yun hivyo akamuita Jack Ma na hapo ndo mwanzo wa kuitwa Jack Ma  mpaka leo.

Jack Ma  alikuwa mpambanaji, hakuwahi kukata tamaa siku zote alikuwa mstali wa mbele kuishi ndoto zake, ilipofika 1994 akapata habari za INTERNET, kwa sababu alipenda sana kujichanganya na watu hivyo akawapata marafiki wazuri walimpenda sana na kumfundisha mambo ya internet📳📟Hivyo naye mbali na kusomea ualimu akaanza kuwa mtaalamu wa internet.

Mwaka 1995 akaondoka na marafiki zake wakaenda Marekani, ndani ya ⓵⓽⓽⓹ wakafungua Ukurasa wa Kibiashara mtandaoni na mpaka mwaka 1998 walikuwa wametengeza zaidi ya Dola 800,000 hapa maisha yake yakaanza kuwa mazuri wakafungua makampuni madogo madogo huko Marekani. Jack Ma  alimiliki kompyuta yake ya kwanza akiwa na miaka 33.

⌚Mwaka 1999 Jack Ma alitengeneza timu ya marafiki 18 na wakarudi China walipofika huko wakaenda nyumbani kwa Jack Ma  na kufungua Kampuni jipya lijulikanalo kama ALIBABA.

Jack Ma  kasomea ualimu lakini aliweza kuanzisha Kampuni na kuliendesha vizuri kampuni,  ambalo limemkweza sana na limemfanya kuwa tajiri wa 21 Duniani kufikia April,2020 akiwa na utajiri wa Dola Bilion 42.3 na kampuni lake limekuwa likifanya vizuri sana Duniani, Kampuni la ALIBABA linajihusisha na maswala ya kuuza bidhaa mtandaoni, kutunza nyaraka na kusambaza filamu na kampuni hili lina zaidi ya thamani ya Dola Bilion 400 na kulifanya liwe moja ya makampuni 20 bora Duniani.

Jack Ma  alipofika 2018 akaomba kuachia ukurugenzi kwa mtu mwingine yeye akarudi kwenye ualimu, kumbuka yeye ndiye mwalimu wa kingereza tajiri zaidi duniani. Na amekuwa akitoa michango mikubwa sana ya maendeleo Duniani Kote.

Ndugu msomaji, mafanikio hayaji kwa bahati nasibu,,,tumeona namna Jack Ma  alipambana sana mpaka kufikia alipo sasa, hivyo sasa  kumbe ili kufanikiwa lazima tujiepushe na kukata tamaa na tuwe makini na marafiki tunaowateneza,  lakini vilevile tuwe na tabia za kuendelea kujifunza na kupambana katika kuishi ndoto zetu,

Jack Ma  alikutana changamoto kibao ikiwa ni pamoja na kukosa kazi na kudharauliwa kumbe kwa mtu anayetafuta mafaniko ni jambo la muhimu sana kuzichukulia changamoto zinazotokea kama fursa za kujifunza na kuuza ubunifu ndio maana Jack Ma  kafikia mafanikio makubwa aliyo nayo mpaka uongozi wa Harvad University ulimfuata nyumbani kuomba afundishe huko chuoni wakati kabla ya kufanikiwa aliwahi kuomba kazi pale mara 10 na kuambiwa hana vigezo.

Tusiogope kujaribu...tukijua kuchekwa, aibu na mengine yote lazima yatokee kwenye safari ya mafaniko.

 Kumbe ndugu mwanafamilia changamoto zako leo ndiyo milango ya mafanikio yako ya badae, Ogopa kupoteza fursa zaidi ya hapo ogopa kukata tamaa kwenye jambo lenye mwonekano wa kuleta faida, umezaliwa kwa ajiri ya ushindi hivyo, kushinda ni jambo la ulazima kwako.


""Thanks Jack Ma (  Ma Yun  )


'''mafanikio hayaji kwa bahati nasibu'''

TUNAKUSHURU KWA KUENDELEA KUWA MWANAFAMILIA  WETU!
Global Family Foundation inajari mafanikio yako


Tunaendelea na kuandikisha watu wenye vipaji mbali mbali kupitia online system,  lengo letu ni kuwa support  iwezekanavyo ili waweze kufikia ndoto zao,, ni sisi tunaofatilia maendeleo yako mwisho wa usajili  utakamilika itakapofika namba ya watu wanaohitajika.  USIKOSE FURSA HII HAITATOKEA
 TENA🎤🎤🎤 ...... 👉 CLICK HERE  to attend online  for your self .

Unaweza  ku-comment!, kuuliza Swali lolote na ku-share.

Ni sisi tunaojali mafanikio yako!



CONTACTS:
phone call:  +255747787796
WhatsApp: Just click👉 HERE   To automatically open whatsApp online service
Website: 👉Click HERE    To open the Site


Email: 👉 Click Here









Comments

  1. Great appreciation to him ( Jack Ma)..
    Hopefully we have got something which concerning with life hustles...

    ReplyDelete
  2. Great appreciation to him ( Jack Ma)..
    Hopefully we have got something which concerning with life hustles...

    ReplyDelete
  3. Asante sana..Global Family Foundation Mnaniongezea tumaini lingine

    ReplyDelete
  4. Dr. Philp MagembeMay 1, 2020 at 2:13 AM

    Congratulations for that vision, we shall discuss something as you come back🙏

    ReplyDelete
  5. I appreciate very much, your global family foundation functions we expect to provide you a great support,,,Please remember to share with us at St. John University when dealing with the CTI project.

    ReplyDelete
  6. Makala zenu, ziko vizuri sana, Naomba muendelee hivy tuko wote

    ReplyDelete
  7. Daniel Kelera PaschalMay 6, 2020 at 3:32 AM

    Huyu bilionea nilikuwa namsikia tuu! Leo nimemjua Nashukuru sana kwa foundation yenu. Tuko pamoja

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

HISTORIA YA SAID SALM BAKHRESA

MAMBO YALETAYO FURAHA YA KWELI MAISHANI

MBINU KUU 4 ZA KUWA MBUNIFU KITAALAMU ZAIDI