Posts

Showing posts from June, 2020

KIJANA MIAKA 18-35 USIKOSE HII

Image
,MAMBO MUHIMU AMBAYO KIJANA ANATAKIWA KUFANYA           Na Prof. Schleiden & Monica Mathias Katika maisha ya binadamu hakuna kipindi kigumu sana kama kipindi cha miaka 20 mpaka  30 kipindi hiki ndio kipindi chenye utata, hapa kijana anaweza kujenga maisha yake au kuyabomoa na walio wengi wanaanguka hapa, lakini pia wengi huanza kufanikiwa kuanzia hapa wote kutegemeana uwezo wao na maono yao yalivyo. ikumbukwe katika miaka 20-30 kijana  ndipo anakuwa anamaliza elimu ya sekondari, ndipo ana anakuwa chuo kikuu , ndipo anaingia kwenye mahusiano ya mapenzi , ndipo anahitimu chuo kikuu, ndipo anaangaika kutafuta ajira , ndipo ana kuwa na mchumba pia ndio kipindi wengine huanza maisha ya kujitegemea kuacha familia za wazazi, wengine hufunga ndoa hapa, pia hiki ni kipindi kijana anaanza kutegemewa na familia ya wazazi wake na jamii. Kwakweli kipindi hiki sio cha mchezo ni kipindi cha kutumia akili nyingi na ushauri mwingi wanao kichukulia poa kinawaachaga vinywa wazi ma